Mamlaka ya Mawasiiano Tanzania (TCRA) imetoza faini mitandao ya simu za mikononi kwa kosa la kusajili laini za simu bila vitambulisho na kutofuata utaratibu uliowekwa na Serikali.
Kampuni zilizotozwa faini hiyo kutokana na kutofuata masharti na kwenda kinyume na utaratibu ni pamoja na Kampuni ya Airtel (Sh1.08 bilioni), Smart (Sh1.3 bilioni), Vodacom (Sh945 milioni), Zantel (Sh105 milioni) na Halotel (Sh1.6 bilioni).
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa TCRA, Mhandisi James Kilaba mapema hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa hii si mara ya kwanza kwa watoa huduma hao kwenda kinyume cha sheria.
Aidha, Kilaba amesema kuwa kutokana na kurudia kosa hilo, TCRA imezitoza kampuni hizo faini ambazo Airtel imetozwa Sh542 milioni, Smart (Sh37 milioni), Tigo (Sh625 milioni), Zantel (Sh52 milioni) na Halotel (Sh822 milioni)
- Dkt. Mpango awatuliza wamachinga, awaahidi makubwa
-
Jaji Mutungi awanyooshea kidole Chadema, CUF
Hata hivyo, ameongeza kuwa kampuni hizo zimetozwa Sh500 milioni kila moja kwa kosa la kuathiri na kuhatarisha usalama wa umma na jamii ya Watanzania kwa kusajili laini bila kufuata utaratibu