Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania TCU imefungua dirisha la maombi ya udahili wa shahada ya kwanza mwaka wa masomo 2020/21.

Akizungumza na waandishi wa habari Katibu Mtendaji wa TCU Profesa Charles Kihampa amesema dirisha la maombi ya udahili wa shahada ya kwanza limefunguliwa kuanzia leo Agosti 26,2020 na litakuwa wazi hadi Septemba 25, mwaka huu.

Aidha Profesa Kihampa amewahasa wanafunzi wanaotarajia kujiunga na vyuo vya elimu ya juu nchini kuepuka kupotoshwa na watu wanaojiita mawakala au washauri wanaodai wanatoa huduma ya jinsi ya kujiunga na vyuo vya elimu ya juu Tanzania.

Profesa Kihampa aongea kuwa, kwa wale waliosoma vyuo vya nje wawasilishe vyeti vyao Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) au Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ili kupata ithibayi ya ulinganifu wa sifa zao kabla ya kuanza kuomba udahili.

Amesema (TCU) imeandaa maonyesho ya 15 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yatakayofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja kuanzia Agosti 31, mpaka Septemba 5 mwaka huu.

Juma Abdul kuvuka Mpaka
Carlinhos ashindwa kucheza 'MAYENU'