Taasisi ya elimu ya juu Tanzania (TCU) imetangaza kuwa kuanzia kesho Agosti 15 saa 6 usiku inatarajia kufunga rasmi dirisha la maombi ya kujinga na masomo ya shahada ya kwanza ambapo kwa mara ya kwanza dirisha hilo lilifunguliwa mnamo Julai 20 kwa awamu ya kwanza.

Hata hivyo kipindi kifupi kilichobaki TCU imesisistiza kuwa waombaji wanatakiwa kusoma muongozo uliotolewa kabla ya kutuma maombi yao ya usaili.

Pia waombaji wanatakiwa kuwasiliana na vyuo wanavyokwenda kusoma ili kupata taarifa kwa kina kuhusu programu za maosomo wanazotarajia kusoma kabla ya kutuma maombi.

Imesema kuwa waombaji wenye vyeti vya nje wanatakiwa kuwasilsiha vyeti vyao katika Baraza la Mitihani Tazania NECTA au NACTE ili kupata idhibati ya ulinganifu wa sifa zao kabla ya kuomba udahili.

Vyuo vikuu na taaissi ya elimu ya juu wanaodahili elimu ya shahada wameleekezwa kuwa na mifumo ya kielektroniki kwa ajili ya kupokea kuchakata na kudahili  ili kurahisiha zoezi hilo.

Na waombaji wanakumbushwa kuzingatia kalenda iliyoidhinishwa na tume.

Aidha Tume ya Vyuo Vikuu imesisitiza kuwa TCU haihusiki na kuwachagulia wanafunzi vyuo bali wanafunzi wenyewe wanachagua vyuo wanavyotaka kusoma kwani kazi kubwa ya TCU ni kuhakiki vigezo husika ambavyo wanafunzi wanatakiwa kuwa navyo ili aweze kuendelea na masomo yake bila kupata usumbufu wowote hapo baade.

 

Wachezaji wamtetea Unai Emery
David Silva afuata nyayo za Iniesta, Pique