Msemaji mkuu wa Tume Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Edward Mkaku ametoa ufafanuzi kuhusu tangazo lililotolewa na Tume hiyo kuhusiana na udahili wa wanafunzi wa vyuo vikuu, amabapo majina na idadi ya wanafunzi katika kila chuo yalitolewa kwa kudahili taarifa zao.
Msemaji huyo alisisitiza kuwa lengo la tume yake halina nia ya kuwafukuza wanafunzi waliorodheshwa kama wengi walivyotafsiri taarifa hiyo bali wanataka kujidhihirisha na kuona kama wanafunzi waliodahiliwa kupitia TCU na NACTE ndio hao ambao wapo vyuoni.
Hivyo Makaku amesema wanafunzi waliotajwa kwenye orodha yao wapeleke nyaraka zao kwa makamu wakuu wa vyuo taaluma, kama walivyoomba na tume hiyo.
Amesisitiza kuwa tume haijatangaza kuwa wanafunzi hao hawana sifa bali wanachotakiwa kufanya ni kupeleka taarifa zao ili kufanya uhakiki wa taarifa hizo.
”katika suala linalohusu vyeti tunakusamehe tu kama huna cheti cha kuzaliwa, kwa sababu tunaamini kwamba ulizaliwa,m lakini kwenye masuala ya elimu vyeti ni muhimu kuwasilisha. Hakuna kosa kumwambia mwanafunzi apeleke cheti,” Amesema msemaji mkuu TCU, edward Mkaku.
Makaku alieleza sababu kuu za kufanya udahili huo alifafanua kuwa baadhi ya wanafunzi hawaonekani kwenye kanzi ya data ya TCU, kutokana na sababu ya kurudia mitihani ya kidato cha nne zaidi ya mara moja.
Hivyo amesema tume imefanya hivyo kwa nia njema na wahusika wote wanatakiwa kufuatilia hilo.