Kampuni ya simu nchini Tanzania ya TECNO imedhamini mashindano ya wanafunzi wanaojifunza lugha na tamaduni za Kichina katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) kwa kushirikiana na taasisi ya Confucius iliyopo chuoni hapo.
Mashindano hayo yamefanyika katika ukumbi wa chuo uliopo katika jengo jipya la maktaba iliyojengwa kwa udhamini wa watu wa china, yalishirikisha takribani washiriki kumi na mbili ambapo wote walikua ni wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam.
Akizungumza wakati wa mashindano hayo, meneja mahusiano wa kampuni hiyo, Eric Mkomoye amesema kuwa TECNO imesaidia kuwapa nafasi vijana wa Kitanzania wanaotamni kutimiza ndoto zao kupitia kujifunza tamaduni za nchi nyingine hasa katika kukuza taaluma zao pia kuweza kuwasiliana na watu wa mataifa mbalimbali.
Aidha, amesema kuwa kampuni yao pamoja na taasis ya Confucius wametoa zawadi mbalimbali ikiwemo simu aina ya spark 3 pia safari ya kwenda nchini China kujifunza zaidi kwa washiriki washindi wawili.
Mashindano ya kuongea Kichina katika chuo kikuu cha Dar es salaam yamefanyika kwa usimamizi mkubwa wa taasisi ya Confucius iliyoanzishwa mwaka 2013 kwa makubaliano kati ya chuo kikuu cha Dar es salaam na makao makuu ya taasisi ya Confucius yaliyopo Hanban na Zhejiang yakihudhuriwa na makamu wa chuo kikuu cha Dar es salaam, Prof. Rutinwa na mkuu wa utamaduni kutoka ubalozi wa China, Gao Wei.
Hata hivyo, Kampuni ya TECNO kwasasa inatangaza simu yake mpya aina ya TECNO Spark 3 imeeendlea kudhamini matukio mbalimbali yanayohusu jamii hasa katika kukuza vipaji vya vijana wa kitanzania na kufanikisha ndoto zao kupitia majukwaa mbalimbali ikiwemo ile maarufu ya kua shujaa wangu.