Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiwa kwenye Jukwaa la Mifumo ya Chakula linalofanyika katika Ukumbi wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, amesema kutumia teknolojia kwenye suala la kilimo kunaenda kurahisisha sekta hiyo kwa vijana.
Mkutano huo, umehudhuriwa na Marais wa nchi 7 wa Afrika, likiwa na lengo la kuongeza uzalishaji wa chakula kwa nchi zao, ambapo amesema serikali yake imewekeza katika suala zima la teknolojia kwa ajili ya kuleta tija kwa wakulima na Watanzania kwa ujumla.
#RaisSamia #KeshoBora #AGRF2023.