Wanasayansi 16 kutoka bara la Afrika wameshiriki katika shindano la kutafuta ufumbuzi kwa changamoto kubwa zaidi zinazoikumba jamii katika bara la Afrika na kuunda programu iliyochukua muda wa takribani miaka mitatu kukamilika .

Shindano hilo limefanyika katika jiji la Kigali nchini Rwanda, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Rais wa nchi hiyo Paul Kagame.

Aidha wanasayansi hao wamezindua programu ya simu itakayotumika na waogonjwa wa ukimwi kufuatilia matibabu yao.

Joel Gasana ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu mjini Kigali na  kiongozi wa timu hiyo amesema programu hiyo itawasaidia wagonjwa wa ukimwi kufuatilia matibabu yao na kudai kuwa walifikia uamuzi wa kutengeneza programu hiyo kutokana na kiwango kikubwa cha maambukizi ya Ukimwi nchini Rwanda na idadi kubwa ya waathirika kutokuzingatia matibabu kama inavyohitajika.

:“Nchini Rwanda, viwango vya maambukizi ya ukimwi vipo juu sana, asilimia 3.3 ya idadi ya watu wameambukizwa, amesema Utafiti uliopo unaonyesha kwamba asilimia 27 ya watu walioambukizwa, hawazingatii matibabu inavyohitajika. Hiyo ndio sababu iliyonifanya kuunda program hii ili kuhakikisha kwamba wagonjwa wote wanazingatia matibabu” amesema Joel

Hata hivyo Rais Paul Kagame alipata nafasi ya kuzungumza amesema, “Kwa mda mrefu, bara la Afrika limekubali kuachwa nyuma lakini hali hii imeanza kubadilika jinsi tunavyoona katika jukwaa hili”

Naye Dr Rose Mutiso, ni mwana teknolojia kuhusu nshati safi amesema, “nadhani ni jambo la kufurahisha na kuchochea kuona kwamba jamii hii ipo, inakua pamoja na kwa ushikamano na tupo sehemu ya jamii ya wanasayansi wa kimataifa

 

Bocco aigalagaza Njombe Mji FC, atumbukiza mawili
Amerika kusini waongoza kununua tiketi za kombe la dunia