Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Morocco Nordin Amrabat, ameonyesha kukasirishwa na maamuzi ya VAR, ambayo kwa kiasi kikubwa yaliamua mchezo wao dhidi ya Hispania na kumalizika kwa sare ya mabao mawili kwa mawili usiku wa jana.
Teknologia ya VAR ilitumika kutoa maamuzi ya bao la kusawazisha la Hispania lililofungwa na Iago Aspas dakika za lala salama, baada ya mwamuzi wa pembeni kuashiria mshambuliaji huyo alikua amezidi/kuotea kabla ya kuukwamisha mpira wavuni.
Maamuzi hayo yaliwakasirisha sana wachezaji wa Morocco na benchi lao la ufundi, lakini dhahir ilibainika kwa Amrabat baada ya kuonyesha kwa vitendo huku akitamka neno zito la kiingireza “VAR is bullshit”.
Hata hivyo inadhaniwa huenda mshambuliaji huyo alifikia hatua hiyo kutokana na baadhi ya matukio waliyofanyiwa wachezaji wa Morocco ndani ya dakika 90 za mchezo dhidi ya Hispania, kutofuatiliwa kwenye teknolojia ya VAR, huku wapinzani wao wakipewa kipaumbele.
Hata hivyo mpaka sasa shirikisho la soka duniani (FIFA) kupitia kamati yake ya nidhamu halijasema lolote kuhusu tukio hilo la Amrabat, ambalo huenda likamuingiza matatizoni.
Kama si maamuzi ya VAR, Morocco huenda wangeweka historioa ya kuifunga Hispania kwa mara ya kwanza katika historia.