Kocha Mkuu wa Manchester United, Erik ten Hag amesemna anaelewa kwa nini mashabiki walizomea mwishoni mwa mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Crystal Palace ambao walifungwa bao 1-0.

Kikosi hicho kinachonolewa na kocha Roy Hodgson kilitoa kipigo cha tano kwa msimu huu kwa United na kusababisha mashabiki kuanza kuizomea timu hiyo.

“Naelewa,” alisema kocha huyo wa Man United.

“Wakati tunacheza nyumbani au ugenini na tunacheza na Crystal Palace, tunatakiwa kushinda. Kwa heshima zote, nafahamu kila mechi Ligi Kuu ya England ni ngumu, unatakiwa kucheza kwa ubora wako na najua mashabiki walitegemea ushindi na hatukushinda, tulipoteza.”

Ni mara ya kwanza tangu mwaka 1989 United imepoteza mechi nne kati ya saba za mwanzo kwenye ligi.

Matokeo hayo yanaiacha timu hiyo ikishika nafasi ya 10 kwenye msimamo wa ligi na kocha huyo kutoka Uholanzi amesema hakuna visingizio na mwanzo wao mbaya kwenye ligi.

“Tunatakiwa kufanya vizuri zaidi ya sasa. Naweza kuwapa sababu lakini mtasema natoa visingizio na hakuna visingizio, tunatakiwa kushinda,” alisema Ten Hag.

Mzize: Mayele amechangia mafanio yangu
Gamondi: Siri yetu kubwa ni ushirikiano