Kocha Mkuu wa Manchester United Erik ten Hag amesema hakuna mgogoro wowote kati yake na Wachezaji wa klabu hiyo, licha ya vichwa vya habari vibaya na msururu wa matokeo mabaya baada ya mabao mawili ya Scott McTominay kuipatia ushindi wa magoli 2-1 Old dhidi ya Chelsea juzi Jumatano (Desemba 06) kwenye Uwanja wa Trafford.

United ilipata ushindi huo licha ya Marcus Rashford kuwekwa benchi umeifanya timu hiyo ya Ten Hag kupunguza tofauti ya pointi hadi tatu dhidi ya mabingwa watetezi Manchester City, ambao wako katika nafasi ya nne baada ya kufungwa 1-0 na Aston Villa.

Lakini huku Ten Hag akiwaacha Rashford na Anthony Martial kufuatia matokeo duni katika mechi ya Jumamosi waliyochapwa 1-0 na Newcastle United, kocha huyo alikataa mapendekezo klabu yake imekuwa katika mgogoro wiki za hivi karibuni.

“Mgogoro? Sio kwa ajili yetu,” alisema Ten Hag.

“Tupo safarini, tumetulia na kuamini mchakato ulivyo, tunajua tunachopaswa kujenga na hatubabaiki na ukosoaji unaotuzunguka, sijali kelele, tunaposhikana tuwe na mtazamo sahihi, tuna mpango madhubuti wa kukusanya pointi.

“Unaona jinsi tulivyoshinda pointi, tulitawala dhidi ya mpinzani wetu kwa kumiliki mpira na hivyo ndivyo tunavyotaka kucheza.”

United walikuwa na mashuti 28, tisa yaliyolenga lango huku walipokuwa wakitawala timu hiyo ya Mauricio Pochettino pale Old Trafford.

Na ingawa bao la Cole Palmer la dakika ya 44 lilisawazisha lile la kwanza la McTominay, kiungo huyo wa United alirejesha uongozi wa timu ya nyumbani na kuipa ushindi kwa bao la kichwa kipindi cha pili.

“Mwishoni tulishinda, lakini tungeweza kurahisisha maisha,” alisema Ten Hag. “Tungeweza kufunga mara tatu katika dakika 30 za kwanza.

“Tunajua hatujaridhika haraka na kuwa na furaha kwa sababu tunataka kufanya vizuri zaidi na kuweka mambo sawa. Lakini nimefurahishwa sana na idadi ya nafasi tulizotengeneza.”

United watawakaribisha Bournemouth kwenye Uwanja wa Old Trafford katika mechi ijayo ya Ligi Kuu England.

TANESCO yafafanua uwepo hitilafu Gridi ya Taifa
Ratiba EPL yamchefua Klopp