Erik ten Hag atapata uhakikisho wa kuwa sehemu ya mipango ya Sir Jim Ratcliffe kwa Manchester United ikiwa bilionea huyo wa England atafikia makubaliano ya kuongoza idara ya michezo ya klabu hiyo, kwa mujibu wa ESPN.
Ratcliffe, mwanzilishi wa Kampuni ya Kemikali ya INEOS, ana matumaini ya kupata asilimia 25 ya hisa za klabu hiyo badala ya uwekezaji wenye thamani ya karibu Pauni Bilioni 1.3.
Ana nia ya kuwa na ushawishi juu ya uendeshaji wa soka, lakini mabadiliko yoyote yaliyopendekezwa hayatajumuisha kuchukua nafasi ya Ten Hag.
Mholanzi huyo aliiongoza United kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu ya England na kushinda Kombe la Carabao katika msimu wake wa kwanza kufuindisha.
Licha ya kuanza vibaya kwa kampeni ya sasa ambapo United wamepoteza mechi sita kati ya 11 katika mashindano yote, Ratcliffe ana mpango wa kumbakisha Ten Hag kama kocha.
United wanatazamiwa kufanya mkutano wa bodi kesho Alhamis (Oktoba 19), Alhamisi wakati makubaliano na Ratcliffe na INEOS yanaweza kukamilishwa.
Ratcliffe anafahamu kuwa ofa yake ya kununua hisa chache inaweza kuwa isiyopendwa na mashabiki kwa sababu bado familia ya Glazer ndio inayoimiliki kwa asilimia kubwa.
Ana matumaini kwamba kwa kupata hisa asilimia 25 ya klabu, itafungua milango ya kuinyakua zaidi angalau kwa muda mfupi.
Mashabiki walikuwa na nia kuona umiliki wa miaka 18 wa Glazers ukiisha ilipotangazwa mnamo Novemba kuwa familia hiyo kutoka nchini Marekani inaweza kuiuza, lakini Jumamosi ilifichuliwa kuwa ofa moja ya udhibiti wa klabu hiyo kwa asilimia l00 kutoka kwa Sheikh Jassim ilikuwa imeondolewa.
Mfanyabiashara huyo wa Qatar alijiondoa katika mchakato huo juma lililopita akitaja hesabu ya “ushabiki” ya Glazers kama sababu kuu.
Ofa ya mwisho ya Sheikh Jassim ilikuwa na thamani ya karibu Pauni Bilioni tano, ikiwa ni pungufu ya Pauni Bilioni moja bei iliyokuwa ikitakiwa na Glazers.