Taasisi za elimu ya juu ndani na nje ya nchi, zimeendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi nchini katika kukabiliana na uhalifu ambapo, Taasisi ya maendeleo ya Jamii Tengeru – TICD, imekua ikishirikiana na taasisi mbalimbali kutoa mafunzo kwa Taasisi za umma na binafsi.

Kauli hiyo, imetolewa leo na Mkuu wa Taasisi ya maendeleo ya Jamii Tengeru Dkt. Bakari George wakati wa kuwasilisha mada mbalimbali katika chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam, amesema kuwa mafunzo hayo yanatolewa wakati chuo hicho kinatimiza miaka 60 katika kutoa elimu juu ya ukatili wa kijinsia.

Dkt. George ameongeza kuwa bado kuna matukio ya ukatili wa kijinsia katika baadhi ya maeneo hapa Nchini ambapo amesema kwa ushirikiano huu ambao umeanza baina ya Jeshi la Polisi na Taasisi hiyo utakwenda kukomesha vitendo vya ukatili katika jamii ya watanzania.

Kwa upande wake Mkuu wa chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam, Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi, SACP Dkt. Lazaro Mambosasa amesema wamejipanga kupokea mafunzo hayo wakufunzi na wanafunzi wa kozi ya uofisa na mkaguzi msaidizi wa Polisi, huku akibainisha kuwa Jeshi hilo litaendelea kushirikiana na taasisi za elimu kukomesha vitendo vya ukatili.

Naye Mkufunzi Mkuu – CI, Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Andrew Legembo amesema mafunzo hayo yataongeza maarifa katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia na watoto hapa nchini ambapo amekishukuru chuo cha maendeleo ya Jamii Tengeru kwa kuwa kinara wa kufundisha masuala ya ukatili wa kijinsia.

Szoboszlai afunguka alivyonasa kwa Klopp
Majaliwa ataka uzingatiaji maadili Viongozi wa umma