Bondia Terence Crawford ambaye alikuwa hajawahi kupigwa katika mapambano yake 28 ameendelea kudumisha rekodi yake baada ya kumtwanga Viktor Postol katika pambano lililofanyika mapema leo asububi katika ukumbi wa MGM Grand Garden Arena nchini Marekani.

Crawford alitawala pambano hilo na kumuangusha chini Postol mara mbili katika ‘round’ ya 5 katika pambano hilo la ‘round’ 12.

Postol ambaye pia alikuwa hajawahi kupigwa katika mapambano yake 27 amelazimika kuandika historia ya kupigwa licha ya kufunzwa vikali na mkufunzi wa bondia Manny Pacquiao, Freddie Roach.

Waamuzi wa pambano hilo wote walimpa ushindi mzito Crawford wa 118-107, 118-107 na 117-108.

“Najisikia kama ninakuwa bora kila siku. Viktor Postol ni mpiganaji bingwa mzuri na alikuwa ananikwepa kwa sababu, lakini mimi sio mtu wa kumkimbia mtu yeyote,” alisema Crawford baada ya pambano hilo.

Zimeanza kutokea tetesi kuwa huenda Crawford akawa amejiweka katika nafasi nzuri ya kukutana ulingoni na Manny Pacquiao kwa mujibu wa promota wake.

Hata hivyo, mshauri wa Manny Pacquiao, aliuambia mtandao wa BoxingScene kuwa Pacquiao hana mpango wa kukutana na Crawford kwani sio ‘size’ yake n ahata kwenye mpango wake hawezi kuingia.

Gwajima amvimbia Makamba
Zitto ampongeza Magufuli, asema Wapinzani wana cha kujifunza CCM