Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), imewasilisha mada juu ya uboreshaji wa Mitaala ya Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Elimu ya Ualimu katika Mkutano Mkuu wa Maafisa Elimu wa Mikoa na Halmashauri (REDEOA).
Mkutano huo ulianza Januari 24 na kufikia tamati mapema Januari 28, katika ukumbi wa Lush Garden Jijini Arusha, ambapo Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dkt. Aneth Komba aliwasilisha mada juu ya uboreshaji wa Mitaala hiyo ya Elimu.
Baada ya wasilisho hilo la Dkt. Komba, Maafisa Elimu hao walipata nafasi ya kupitia na kutoa maoni yao juu ya uboreshwaji wa Mitaala hiyo.
Mkutano huo ulikuwa na kauli mbiu inayosema; “Kuboresha miundombinu ya Shule na kuimarisha Elimu kwa Maendeleo Endelevu na kukuza uchumi wa Taifa”
Zoezi hili la ukusanyaji wa maoni linatarajiwa kukamilika tarehe 31/01/2022 ambapo mchakato wa kuboresha Mitaala itachukua muda wa miaka 3 na Mitaala mipya inatarajiwa kuwa darasani mwaka 2025.