Tasisi ya Elimu Tanzania (TET), imewasilisha mada juu ya uboreshaji wa Mitaala ya Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Elimu ya Ualimu katika Mkutano Mkuu wa Maafisa Elimu wa Mikoa na Halmashauri (REDEOA).
Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dkt. Aneth Komba aliwasilisha mada juu ya uboreshaji wa Mitaala hiyo ya Elimu, ambapo mitaala hiyo ni pamoja na Mitaala ya Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Elimu ya Ualimu.
Baada ya wasilisho hilo la Dkt. Komba, Maafisa Elimu hao walipata nafasi ya kupitia na kutoa maoni yao juu ya uboreshwaji wa Mitaala hiyo.
Mkutano huo wenye kauli mbiu ya; “Kuboresha miundombinu ya Shule na kuimarisha Elimu kwa Maendeleo Endelevu na kukuza uchumi wa Taifa”
Zoezi hili la ukusanyaji wa maoni linatarajiwa kukamilika tarehe 31/01/2022 ambapo mchakato wa kuboresha Mitaala itachukua muda wa miaka 3 na Mitaala mipya inatarajiwa kuwa darasani mwaka 2025.
credit @tbc