Idadi ya vifo kufuatia tetemeko la Ardhi nchini Morocco imefikia karibu watu 2,900 huku wengine zaidi ya 2,500 wakiwa wamejeruhiwa, huku Vikosi vya uokoaji vikiendelea kuwatafuta manusura, huku Morocco ikikosolewa kwa kuchelewa kutoa idhini kwa mashirika mengine ya uokoaji kuingia nchini humo, ili kutoa msaada.
Hata hivyo, Maafisa wa Morocco wamejitetea wakidai kuwa uamuzi huo wa ucheleweshaji unalenga kuepuka mkanganyiko katika uratibu ambao wanadai hautokuwa na manufaa yoyote.
Ufaransa imetangaza msaada wa dharura kwa Morocco wa dola milioni 5.4 utakaolekezwa kwa mashirika ya kimataifa yasiyo ya kiserikali yanayoendelea kutoa msaada nchini humo.
Tetemeko hilo, ni tukio baya zaidi kuwahi kuikumba nchi hiyoya Kaskazini mwa Afrika tangu tetemeko la ardhi la mwaka 1960 lililoharibu mji wa Agadir na kusababisha vifo vya maelfu ya watu.