Klabu ya Al Ittihad Tripoli ya Libya ipo mboni karibu kufanikisha mpango wa mshambuliaji wa Tanzania, Adam Omar Adam. 

Mshambuliaji huyo tegemezi wa kikosi cha JKT Tanzania kinachoshirik Ligi Kuu Tanzania Bara amefunga mabao saba katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

Klabu ya Al Ittihad Tripoli ambayo ni bingwa wa soka nchini Libya,  hakuwahi kutajwa hapo awali katika mchakato wa kumuwinda mshambuliaji huyo, ambaye aliwahi kwebnda nchini Uturuk kufanyiwa majaribio.

Huenda harakati za Adam Adam kuelekea nchini Uturuki ziliwafanya viongozi wa klabu ya Al Ittihad Tripoli, kuanza kumfuatilia na kuona atawafaa kwenye kikosi chao, hasa katika kipindi hikia mbacho wanapambana kurejesha heshima barani Afrika.

Al Ittihad ni mabingwa wa kihistoria nchini Libya wakibeba taji la Ligi Kuu mara 16 na pia kutinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika mwaka 2007 na 2010.

Bumbuli: Kesho kikosi kitakua kamili
Ligi Kuu kuendelea April 08