Arsenal ina hamu ya kumsajili kungo wa kati wa Olympic Lyon na Ufaransa Houssem Aouar 22, lakini inakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Paris St-Germain na Juventus. (Tuttosport – Italian)
Meneja wa Arsenal Mikel Arteta anasema kwamba amekuwa wazi na kiungo wa kati wa Ujerumani Mesut Ozil, 32, licha ya wakala wa mchezaji huyo kudai kwamba kumekuwa hakuna uwazi kuhusu mchezaji huyo kuwachwa nje ya kikosi cha timu hiyo. (The Mirror)
- Manchester United ilikosa kumsajili beki wa RB Leipzig na Ufaransa mwenye umri wa miaka 21 Dayot Upamecano – ambaye kwa sasa ana thamani ya £55m – kwasababu ya mgogoro kuhusu £200,000 miaka mitano iliopita . (Sun)
- Liverpool Huenda ikaamua kutomsaini beki wa kati mwezi Januari na kusubiri mchezaji atakayedumu msimu ujao, licha ya jeraha baya lililompata beki wa Uholanzi Virgil van Dijk. (Liverpool Echo)
- Kiungo wa kati wa Real Madrid na Croatia Luka Modric, 35, amesisitiza kwamba yeye ni mzee sana kufuata nyayo za mshambuliaji wa Wales Gareth Bale na kurudi Tottenham.. (FourFourTwo via Marca)
- Winga wa Manchester City na Algeria Riyad Mahrez, 29, amekana madai katika vyombo vya habari vya Ufaransa kwamba alizungumzia uwezekano wa kujiunga na PSG.
- Mshambuliaji wa Ufaransa, Kylian Mbappe, 21, amekusudia kuipatia klabu yake ya Paris Saint-Germain Football Club ubingwa wa Champions League kabla ya kuhamia kwenye timu nyingine kubwa maneno hayo ni kulingana na kiungo wa kati aliyeichezea PSG na ambaye sasa ni balozi wa klabu hiyo Youri Djorkaeff. (Goal)
- Mshambuliaji wa Juventus na Argentina Paulo Dybala 26 ambaye amehusishwa na uhamisho wa kuelekea Tottenham pamoja na Man United yuko katika mazungumzo ya kuandikisha mkataba mpya na klabu hiyo ya Itali. (Sky Sports)
- Mshambuliaji wa Poland Arkadiusz Milik, ambaye alikuwa tayari kujiunga na Juventus msimu ujao ataondoka SSC Napoli mwezi Januari huku klabu za Tottenham na Everton zikimnyemelea mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26. (Calciomercato via Mail).
- Klabu ya Sheffield United wanataka kumchukua beki wa Man United na Argentina Marcos Rojo 30, kwa mkopo mwezi Januar. (The Sun)