Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC wanahusishwa na mpango wa kuanza mazungumzo na Nahodha na Beki kati wa klabu ya Young Africans, Bakar Nondo Mwamnyeto.

Taarifa kutoka ndani ya Uongozi wa klabu hiyo zimethibitisha kuwa Uongozi umedhamiria kuipata saini yake huku ikifahamika kuwa kesho Jumatano (Februari 02), huenda ukafanya mazungumzi na meneja wa mchezaji huyo Kasa Musa.

Simba SC pia bado wamemng’ang’aninia kiraka wa Yanga SC Kibwana Shomari ambao wote kandarasi zao zinaisha mwisho wa msimu huu.

Hata hivyo Klabu ya Simba SC haijazungumza lolote kuhusu mpango huo kwa wachezaji wote wawili, zaidi ya kuendelea kuzungumza kama Tetesi katika mitandao ya kijamii.

Zuhura Yunus Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu
Abdallah Bacca akabdhiwa jukumu Young Africans