Wakala wa Lucas Torreira amefika Madrid, Hispania kufanya mazungumzo na Atletico Madrid juu ya uwezekano wa kiungo huyo wa kati mwenye umri wa miaka 24, raia wa Uruguay kuondoka Arsenal.

  • Chelsea iko tayari kumuuza mlinzi wa Ujerumani Antonio Rudiger na ingawa Tottenham pia inamkodolea macho mchezaji huyo, 27, ingependelea ikiwa angehamia nje ya Uingereza.
  • Pep Guardiola anataka kumsajili beki wa kushoto mpya kabla ya dirisha la usajili kufungwa na David Alaba wa Bayern Munich na Austria, pamoja na mchezaji wa Ajax na Argentina Nicolas Tagliafico, wote wakiwa na umri wa miaka 28, wakinyatiwa na Manchester City.
  • Mabingwa wa Ujerumani FC Bayern Munich wamewasiliana na Brighton juu ya uwezekano wa makubaliano na beki wa kulia Tariq Lamptey, 19.
  • Beki wa kulia wa Brazil Thiago Silva, 36, anasema “alikasirishwa” na vile Paris St-Germain ilivyoshughulikia kuondoka kwake, na hata ikiwa mabingwa hao wa Ufaransa waliomuongezea mkataba wa mwaka mmoja muda ulikuwa umekwenda kwasababu tayari alikuwa amekubali kujiunga na Chelsea.
  • Ofa ya Manchester United ya pauni milioni 91.3 kwa ajili ya mshambuliaji wa England Jadon Sancho, 20 imekataliwa na Borussia Dortmund.
  • Manchester United inakaribia kufanikiwa kumsajili mshambuliaji wa Barcelona na Ufaransa Ousmane Dembele, 23, – wakiipiga Barcelona jeki kifedha kumsajili mshambuliaji wa Lyon aliyekuwa Manchester United Memphis Depay.
  • Southampton huenda ikachukua hatua ya kuchelewa kumsajili kiungo wa kati wa Heerenveen Uholanzi Joey Veerman.
  • Ofa ya West Ham ya mkopo kwa beki wa kulia Vladimir Coufal, 28, wa timu ya Slavia Prague ya Jamhuri ya Czech imekataliwa.

Mosimane awatema Masandawana
Kwa kauli hii, Manchester United hawana chao