Wakati janga la virusi vya Corona likizidi kutikisa sekta ya michezo na sekta nyingine duniani, klabu mbalimbali zimeendelea na mipango kadhaa ya usajili kwa ajili ya kujiimarisha na msimu ujao 2020/21.
Klabu za soka nchini England, zimeendelea kuchukua nafasi kubwa katika mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari kwa kuhusishwa na harakati za usajili, kwa kufikiria kuwauza wachezaji na kuwanunua watakaokua mbadala.
Licha ya tetesi za usajili kuendelea kupewa nafasi kubwa katika mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari, bado sintofahamu ya kuendelea kwa ligi za mataifa mbalimbali duniani inaendelea kushika hatamu.
Zifuatazio ni sehemu ya taarifa zilizopewa nafasi kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari kuhusu tetesi za usajili wa wachezaji.
Manchester United huenda wakalazimika kumuuza kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 27, kwa bei ya chini kutokana na athari za janga la corona katika mchezo wa soka. (Goal).
Arsenal watamuuza mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30, kwa dau la £30m kwasababu hawataki aondoke klabu hiyo kwa uhamisho wa bila malipo. (Sun).
The Gunners bado haijampatia mkataba mpya kiungo wa kati wa Ujerumani Mesut Ozil, 31. (ESPN).
West Ham inatarajiwa kukataa ofa iliyowasilishwa na Chelsea ya kumnunua kiungo wa kati wa England Declan Rice, 21. (Goal).
Newcastle na Everton wanang’ang’ania saini ya kiungo wa kati wa Ajax na Netherlands Donny van de Beek. Manchester United na Real Madrid pia wamehusishwa na nyota huyo wa miaka 23. (Le10 Sport – in French).
Everton wamempatia ofa ya mkataba wa miaka minne kiungo wa kati wa Real Madrid na Colombia James Rodriguez, 28. (Mundo Deportivo – in Spanish).
Arsenal na Manchester United wanataka kumsajili mshambuliaji wa Monaco na Ufaransa Wissam Ben Yedder, 29. (L’Equipe – in French).
Everton imefanya mazungumzo na Barcelona kumhusu beki wa miaka 20 Jean-Clair Todibo. Kinda huyo wa Ufaransa sasa yupo Schalke kwa mkopo. (Mail).
Liverpool imeanza mazungumzo na wawakilishi wa mshambuliaji wa Lille na Nigeria Victor Osimhen, 21. (Le10 Sport – in French).
Newcastle wanapania kumbadilisha mkufunzi wao Steve Bruce with Flamengo na Jorge Jesus, ambaye aliongoza klabu hiyo ya Brazil mwaka 2019 kushinda taji la Copa Libertadores. (Goal).
Arsenal italazimika kuilipa Real Madrid euro milioni 50 sawa na (£44m) wakitaka kumsaini kwa mkataba wa kudumu kiungo wa kati wa Uhispania Dani Ceballos, 23, ambaye anachezea klabu hiyo kwa mkopo. (AS – in Spanish).
Arsenal wanajizatiti kumzuia winga wao wa miaka 18, Bukayo Saka anayenyatiwa na klabu zingine za Ligi ya Primia asiondoke, kwa kumpatia mkataba mpya. (90min).
Chelsea wanataka kumsaini kiungo wa kati wa Paris St-Germain Mfaransa Kays Ruiz-Atil,17, ambaye mkataba wake unamalizika 2021. (L’Equipe – in French).