Manchester United wamemuulizia ‘kimyakimya’ mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane, 22 na watafanya maombi rasmi iwapo Spurs watakubali (Daily Mirror)

Manchester City wanaamini kuwa watakamilisha uhamisho wa kiungo wa Wolfsburg Kevin De Bryne, 24 kabla hawajacheza na Chelsea siku ya Jumapili (Daily Mail)

Chelsea wataongeza dau lao la pauni milioni 30 kumtaka beki wa kati John Stones, 21, kutoka Everton (Daily Mirror)

Meneja wa Everton¬†Roberto Martinez amesema Stones ni “professional” ambaye “hatozira” iwapo uhamisho wake kwenda Chelsea hautafanikiwa (Guardian)

West Ham watawapa Manchester United pauni milioni 12 kumsajili Javier Hernandez baada ya kukataliwa dau la mwanzo la pauni milioni 8 (Daily Star)

Beki wa kushoto wa Everton Leighton Baines, 30, huenda asicheze kwa miezi mitatu baada ya kufanyiwa upasuaji wa mguu wiki hii (Daily Express)

Kipa wa Manchester United David De Gea amesema alikuwa tayari kucheza dhidi ya Tottenham siku ya Jumamosi, licha ya Louis van Gaal kudai kuwa hakuwa tayari kutokana na tetesi za kuhamia Real Madrid (Daily Mail)

Meneja wa Manchester City Manuel Pellegrini anaamini Raheem Sterling anaweza kufika thamani ya pauni milioni 100 siku za usoni (Manchester Evening News)

Pellegrini amekiri kuwa kazi yake itakuwa mashakani kama hatoshinda Ligi Kuu msimu huu (Sun), beki kutoka Argentina Martin Demichelis, 33, anaamini Manchester City wana nafasi kubwa ya kushinda ligi msimu huu (Sky Sports)

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amekataa kumrushia lawama kipa Petr Cech, 33, kwa jinsi alivyocheza katika mechi waliyopoteza 2-0 dhidi ya West Ham (Daily Star)

Meneja wa zamani wa Tottenham na QPR Harry Redknapp anaamini kuwa Arsenal wanaweza kushinda ligi licha ya kupoteza mechi ya kwanza, lakini ikiwa watasajili mshambuliaji mwingine (Daily Telegraph).

 

Neymar Nje Siku 14
Tenga, Malinzi Waula CAF