Manchester City wanafikiria kumsajili kwa mkopo kiungo wa Brazil Douglas Luiz, 26, ingawa Juventus inashinikiza wajibu wa kumsaini ili kujumuishwa katika mpango huo uliopendekezwa. (Athletics)
Vilabu vya ligi ya Saudi Arabia bado vina nia ya kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Vinicius Jr, 24, nchini humo – huku mtendaji mkuu wa ligi hiyo akisema kuhama ni “suala la muda”. (ESPN)
Chelsea wanataka pauni milioni 40 kumuachilia beki Muingereza Trevoh Chalobah baada ya kumrejesha mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 25 kutoka Crystal Palace. (Sun)
Mchezaji mwingine wa Chelsea, Cesare Casadei mwenye umri wa miaka 22, huenda akaelekea Lazio baada ya vilabu hivyo viwili kukaribia kuafikiana. (Sky Sports Italia)
Mechi ya Jumapili ya Man United dhidi ya Brighton inatarajiwa kuwa mchezo wa mwisho kwa winga wa Brazil Antony, 24, akiwa amevalia jezi ya klabu hiyo, baada ya makubaliano ya awali kuhusu uhamisho wake wa mkopo kuelekea Real Betis. (Fabrizio Romano)
Kocha wa zamani wa Manchester United Erik ten Hag anaweza kuchukua nafasi ya Nuri Sahin kama mkufunzi wa Borussia Dortmund ikiwa klabu hiyo itashindwa katika mechi yao ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Bologna siku ya Jumanne. (Florian Plettenberg, Sky Sports Germany)
Manchester United na Chelsea watachuana na Bayern Munich kumsaini kiungo wa Uingereza Jamie Gittens, 20, majira ya kiangazi. (Florian Plettenberg, Sky Sports Germany)
Real Madrid wako tayari kusitisha azma yao ya kumsaka beki wa Canada Alphonso Davies, 24, ambaye anakaribia kufikia makubaliano ya kuongeza mkataba wake Bayern Munich. (AS – kwa Kihispania)
Juventus wana nia ya kusajili mlinzi wa Newcastle Lloyd Kelly, 26, – miezi saba tu baada ya mchezaji huyo kuwasili kutoka Bournemouth kwa uhamisho wa bure. (Gianluca di Marzio)