Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeungana na Uongozi wa Young Africans kwa kulaani kitendo kilichofanywa na kocha Luc Eymael baada ya sauti yake yenye ujumbe wa ubaguzi kusambaa katika mitandao ya kijamii, pamoja na vituo mbalimbali vya habari.

TFF imekwenda mbali zaidi kwa kuahidi kumfikisha kocha huyo kutoka Ubelgiji kwenye chombo cha juu cha soka duniani (Shirikisho La Soka La Kimataifa FIFA.

Kocha Eymael anaondoka Young Africans baada ya kuiongoza timu katika michezo 32 tangu ajiunge nayo Januari ikishinda 16, sare 11 na kufungwa tano.

Anaondolewa siku moja baada ya kuisaidia Young Africans kumaliza katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kufuatia ushindi wa bao moja kwa sifuri  dhidi ya wenyeji, Lipuli FC jana Uwanja wa Samora mjini Iringa, bao pekee, David Molinga Ndama ‘Falcao’ dakika ya 38.

Kwa ushindi huo, Young Africans imefikisha alama 72 na kumaliza nafasi ya pili ikizidiwa alama 16 na mabingwa, Simba SC na wakiwazidi alama mbili Azam FC waliomaliza nafasi ya tatu.

China: Ubalozi mdogo wa Marekeni wafungwa
Luc Eymael atimuliwa Young Africans