Hatimaye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kupitia Bodi ya Ligi (TPLB) limetangaza makundi matatu ya timu zitakazoshiriki Ligi Daraja la Kwanza kwa msimu wa 2016/17.

Kitimtim cha Ligi hiyo ya StarTimes kimepangwa kuanza Agosti mwaka huu baada ya kukamika kwa michakato ya usajili unaoanza Juni 15 mwaka huu.

Tarifa ya TFF kwa vyombo vya habari imeyataja makundi hayo matatu kila moja likiwa na timu nane (8), kwa alama ‘A’, ‘B’ na ‘C’

Hiki ndicho kitimtim kinachotarajiwa kutimka mwaka huu katika makundi:

Kundi A
1 Abajalo ya Dar es Salaam
2 African Sports ya Tanga
3 Ashanti United ya Dar es Salaam
4 Kiluvya United ya Pwani
5 Friends Rangers ya Dar es Salaam
6 Lipuli ya Iringa
7 Mshikamano FC ya Dar es Salaam
8 Polisi Dar ya Dar es Salaam

Kundi B
1 JKT Mlale ya Ruvuma
2 Coastal Union ya Tanga
3 Kimondo FC ya Mbeya
4 Kinondoni Municipal Council ya Dar es Salaam
5 Kurugenzi ya Iringa
6 Mbeya Warriors ya Mbeya
7 Njombe Mji ya Njombe
8 Polisi Morogoro ya Morogoro

Kundi C
1 Alliance Schools ya Mwanza
2 Mgambo Shooting ya Tanga
3 Mvuvumwa FC ya Kigoma
4 Panone FC ya Kilimanjaro
5 Polisi Dodoma ya Dodoma
6 Polisi Mara ya Mara
7 Rhino Rangers ya Tabora
8 Singida United ya Singida

Viongozi wa mfuko wa Pamba wameumbuliwa
Video: Alichokisema Zitto Kabwe baada ya polisi kuzuia Kongamano la Bajeti