Baada ya kutekeleza ahadi ya mwanzo ya kuipeleka Madagascar kwa ajili ya kambi ya kuivaa Afrika Kusini ‘Amajimbos’, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amepanga kutekeleza ahadi yake nyingine kwa kuipeleka timu ya taifa ya Tanzania ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ kwenye kambi tulivu, ikiwezekana nje ya nchi.

Rais Malinzi aliahidi na kutekeleza ahadi yake kuipeleka Madagascar Serengeti Boys baada ya kuitoa Shelisheli katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika Madagascar, mwakani. Kadhalika aliahidi kuipeleka timu hiyo nje ya nchi ambayo hata hivyo haijateuliwa baada ya kuindoa Afrika Kusini. Ameahidi kambi hiyo itaanza Septemba mosi, mwaka huuu.

Serengeti Boys ilipiga kambi Hosteli za TFF, zilizo Karume kwa wiki moja kabla ya kuhamia Hoteli ya Urban Rose, katikati ya jiji la Dar es Salaam ambako ilivunjwa kwa muda jana Agosti 22, 2016 ambako vijana wamekwenda makwao kusalimia ndugu zao na itaitwa mwishoni mwa mwezi huu kwa ajili ya maandalizi ya kambi ya nje ya nchi.

Serengeti Boys imebakiwa na mtihani mmoja kufuzu kucheza fainali hizo kwa kucheza na Congo – Brazaville na mchezo wa kwanza utafanyika Dar es Salaam, Septemba 18, 2016 kabla ya kurudiana Septemba 30, 2016, Oktoba 1 au Oktoba 2, 2016.

TFF imejipanga kwa ajili ya kambi hiyo, na kinachosubiriwa kwa sasa ni mapendekezo ya makocha ili shirikisho itekeleze hatua hiyo ya kambi ya utulivu.

Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Bakari Shime maarufu kama Mchawi Mweusi amesema kwamba anaamini kuwa mchezo ujao utakuwa mgumu kwa kuwa kila timu nitajipanga kuvuka ili kucheza fainali hizo.

FC Barcelona Wamuongezea Muda Wa Mapumziko Neymar
Waziri Mkuu akagua ujenzi wa daraja mto Kavuu