Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupitia kwa Rais wake, Jamal Malinzi ametuma salamu za pongezi kwa klabu ya Ruvu Shooting kwa kufanikiwa kupanda Ligi Kuu ya Vodacom msimu ujao.

Malinzi ametuma salamu hizo kwa Mwenyekiti wa klabu ya Ruvu Shooting, Col. Charles Mbuge, viongozi, benchi la ufundi na wachezaji na kuwataka kujipanga kwa maandalizi ya nguvu msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom.

Ruvu Shooting imekua timu ya kwanza kupanda ligi kuu msimu huu baada ya jana kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Lipuli FC mjini Iringa na kufikisha alama 31 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote kutoka katika hilo la B.

Washindi wawili kutoka maundi ya A, na B wataungana na Ruvu Shooting kupanda Ligi Kuu ya Vodacom msimu ujao huku timu zote zikiwa zimebakiza michezo miwili miwili kabla ya kumalizika kwa ligi daraja la kwanza msimu huu.

Jaji Lubuva akutana na Rais Magufuli, asema Rais hawezi kuingilia uchaguzi Zanzibar
Simba Yaandika Historia Mpya