Rais wa Shirikisho la Soka nchini TFF, Wallace Karia amesadikika kuwa ametoa kauli iliyoleta utata kuhusiana na zuio la mashindano ya soka yasiyo rasmi, ambapo TFF limetoa ukanusho wa taarifa hiyo na kufanya ufafanuzi wa ziada.

Shirikisho hilo la Soka nchini limeeleza kuwa alichosema Rais uyo ni kuhusiana na maandalizi ya kanuni ambazo zitatakiwa kufuatwa na waandaji wa mashindano madogo ya soka nchini na si zuio la mashindano kama ambavyo ilitafsiriwa na jopo la watu.

“TFF inaandaa kanuni ili mashindano yote ya aina hiyo yakidhi vigezo katika utaratibu mzuri na watapata vibali kupitia FA Wilaya na Mikoa baada ya kutimiza vigezo vitakavyowekwa”, imeeleza sehemu ya taarifa ya TFF.

 

Video: Alichozungumza Kakobe, asakwa kwa mahojiano
Matokeo ya mtihani wa kidato cha nne 2017 pasua kichwa