Shirikisho la soka nchini TFF limekanusha taarifa za kuachana na Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa Taifa Stars Kim Polusen na kumuajiri Jamal Sellami, kutoka nchini Morocco.
TFF wametoa taarifa inayoeleza kuwa, Kim Poulsen bado ni Kocha Mkuu wa Taifa Stars, na wameshangazwa kuibuka kwa taarifa za kuondolewa kwa kocha huyo kutokla nchini Denmark.
Taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zilieleza kuwa, TFF wameachana na Kim Poulsen na kuingia mkataba ba Kocha Sellami ambaye kwa sasa ni Kocha Mkuu wa klabu ya Raja Casablanca.