Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) chini ya mwenyekiti wake, wakili Richard Sinamtwa imeliidhinisha jina la mchezaji Hassan Kessy kuichezea Young Africans huku akitakiwa kuilipa klabu yake ya zamani, Simba SC kwa kuvunja Mkataba.

Kessy anatakiwa kuilipa Simba SC Sh. Milioni 120 ili aanze kuichezea timu yake mpya ya Young Africans katika mashindano kuanzia sasa.

Taarifa hizo zinaeleza kuwa katika mkataba wake na Simba, wote klabu na mchezaji walikubaliana atakayeuvunja atalipa dola za Kimarekani 60,000 zaidi ya Sh. Milioni 120,000 za Tanzania.

Kessy alisajiliwa na Simba SC misimu miwili iliyopita kutoka Mtibwa Sugar ya mkoani Morogoro kwa Mkataba wa miaka miwili akilipwa Sh. Milioni 20.

Lakini taarifa kutoka Young Africans zinasema kuwa klabu hiyo haipo tayari kulipa Sh. Milioni 120 ambazo Simba wanataka ili Kessy acheze  maana yake beki huyo anaweza kuendelea kubaki benchi.

Mahakama yamtaka Mengi kujitetea kwanini asifungwe kwa madai
Victor Valdes: Nilipokua Man Utd, Nilitamani Kustaafu Soka