Shirikisho la soka nchini (TFF), limeongeza muda zaidi kuimarisha idara zake ambako imeongeza muda wa wiki moja kwa Watanzania wenye sifa za Idara ya Masoko na Habari ili kuongoza Idara hiyo.

Awali tarehe ya  mwisho ilikuwa Julai 11, 2016 lakini kwa sasa tarehe ya mwisho itakuwa Julai 19, mwaka huu kwa nafasi ambazo TFF imetangaza ajira.

Lengo hasa ni kuendana na hali halisi ya uendeshaji mpira wa miguu duniani ambako masoko, habari na mahusiano ya Kimataifa yamekuwa funguo za kupata rasilimali kwa ajili ya maendeleo ya mchezo wa mpira wa miguu popote duniani.

Pili ni kuhakikisha rasilimali za kuendesha mpira wa miguu zinatokana na soka na vilevile kuhakikisha wadau wanapata habari sahihi kwa wakati mwafaka.

Kwa nafasi za kazi TFF tembelea tovuti yao www.tff.or.tz au waandikie ili utumiwe tangazo kwa barua pepe tanfootball@tff.or.tz

Mbali ya kuboreshwa kwa Idara hiyo ya Masoko, pia TFF imepania kutoa kipaumbele katika masuala ya waamuzi na wanawake kwa kuanzisha madawati ya kudumu katika Kurugenzi ya Ufundi. Hapo awali madawati ya wanawake na waamuzi yaliendeshwa na watumishi wa kujitolea (Volunteers) au wa muda (Part timers).

Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine aliamsha changamoto mbalimbali za soka la wanawake miongoni mwanzo ikiwa ni uibuaji na uendelezaji vipaji, Timu ya Taifa, mafunzo katika taaluma mbalimbali, ligi za wanawake na masoko kwa bidhaaa (products) za soka la wanawake.

Kuhusu waamuzi, Katibu Mkuu alilielezea eneo hili kama lenye changamoto nyingi hasa hasa katika kupata waamuzi wenye viwango vya Kimataifa.

Shirika La Ndege La Kenya Kuwaleta Wapinzania Wa Young Africans
Mohamed Mustapha na Wenzake Kortini kwa Kuiletea Serikali Hasara ya Bil.15