Shirikisho la soka nchini TFF limekanusha uwepo wa akaunti ya mtandao wa Twitter inayosomeka kwa jina la Rais wa shirikisho hilo Wallace Karia.

TFF wametoa taafira hiyo kupitia kitengo cha habari na mawasilino kinachoongozwa na Alfred Lucas, baada ya kuona kuna upotoshaji unaoendelea kusambazwa katika mitandao ya kijamii kw alengo la kuchafua jina la Karia.

“Kuna Akaunti mpya wa Twitter inazunguka katika mitandao ya kijamii. Akaunti hiyo yenye jina la Rais wa Shirikisho l Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imeanza kutoa taarifa mbalimbali na kuchangia maoni kunakoelezwa kufanywa na Wallace Karia. TFF tunatangaza kuwa hatuitambui akaunti hiyo. Rais Karia hajafungua akaunti ya Twitter.”

“Tunaomba wananchi wote hususani wanafamilia wa mpira wa miguu, kutoitambua akaunti hiyo kwa sababu si ridhaa ya Rais Karia wala Kitengo cha Habari TFF kilichofungua akaunti hiyo.” Imeeleza taarifa ya TFF

Hata hivyo haikuelezwa ni maoni gani ambayo yameshagiwa kupitia kaunti hiyo feki yenye jina la Wallace Karia.

 

Kenyatta awataka NASA kwenda mahakamani
RC Rukwa awataka watumishi wa umma kutobweteka