Shirkisho la Soka nchini Tanzania ‘TFF’ limetaja vituo vitakavyotumika kwa ajili ya michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) hatua ya makundi, inayotarajiwa kuanza Machi 4.

Mkuu wa Idaya ya Habari na Mawasilino ya TFF Cliford Mario Ndimbo amesema vituo hivyo ni Arusha, Pwani, Lindi na Katavi, na kila kituo kitakua na timu saba.

Ndimbo amesema maandalizi ya michuano hiyo inaendelea vizuri na TFF inatarajia ushindani wa kweli kutoka kwa timu zote 28 zitakazoshiriki mchuano hiyo mwaka huu 2021.

Kituo cha Arusha kitakuwa na timu za Kundi A ambazo ni wenyeji TMA Stars, Sinai Rangers (Manyara), Sharp Strickers (Tanga), TRA (Kilimanjaro), Mara Sports Academy (Mara), Copco Veteran (Mwanza) na Huduma FC (Dar es Salaam).

Kundi B kituo cha Pwani kuna wenyeji Baga Friends, Temeke Squad (Dar es Salaam), 515 KJ (Morogoro), Manyoni Sports Center (Singida), Kimara United (Dodoma), Annuary FC (Shinyanga) na Bariadi United (Simiyu).

Kundi C kituo cha Lindi kuna wenyeji Lindi United, Mkuti Market (Mtwara), Mabomba FC (Dar es Salaam), Top Boys FC (Ruvuma), Njombe Academy (Njombe), Mtwivila FC (Iringa) na Itezi FC (Mbeya).

Kituo cha Katavi cha Kundi D kitakuwa na wenyeji timu ya Tanesco FC, Sumbawanga United (Rukwa), Mapinduzi FC (Songwe), Black Stars (Tabora), Toto Kigoma FC (Kigoma), Nyaishozi FC (Kagera) na Nyakumbu FC (Geita).

Barbara: Kazi ndio imeanza Simba SC
Tambwe: Young Africans hawajanilipa fedha zangu