Shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) limeweka wazi kwa kuipandisha Tanzania kuwa kwenye nafasi ya nchi 12 zitakapoleka timu nne katika michuano ya kimataifa msimu ujao wanatoisimamia upande wa ngazi ya klabu.

Hiyo ni kufuatia Simba SC kufika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu na kuwapiga bao Libya.

CAF imeipandisha Tanzania kuwa miongoni mwa nchi 12 ambazo zinapeleka timu nne msimu ujao wa 2021/22 ambapo mbili zitashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika na zingine Kombe la Shirikisho Afrika.

Kwa mujibu renki za CAF, Tanzania imepanda hadi nafasi ya 12 ikiishusha Libya iliyokuwa katika nafasi hiyo ambayo imeteremshwa kwa nafasi tatu ikiwa pointi 13.5.

Kitendo cha Simba kufika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu, kimeifanya Tanzania kukusanya pointi 27.5.

Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka Tanzania TFF, Salum Madadi ambaye amefafanua juu ya timu ambazo zitakuwa na nafasi ya kushiriki michuano hiyo.

“Nafasi ya kupeleka timu nne namna ilivyo ni kwamba, mbili zitatoka kwenye ligi kuu kwa maana ya mshindi wa kwanza na wa pili, na zingine mbili katika Kombe la FA kwa zile ambazo zimecheza fainali.”

“Lakini ikitokea bingwa wa ligi kuu ameingia fainali ya Kombe la FA, basi atakwenda kuiwakilisha nchi kwenye Ligi ya Mabingwa halafu mshindi wa pili wa FA atakwenda Kombe la Shirikisho Afrika, baada ya hapo mshindi wa pili wa ligi atakwenda Ligi ya Mabingwa na mshindi wa tatu atacheza Shirikisho,” amesema Madadi.

Kauli ya Azam FC

Mkuu wa Idara ya Habari ya Azam, Thabit Zakaria ‘Zaka za Kazi’, amezungumzia suala hilo akisema kwa upande wao walishajiandaa mapema kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao.

“Binafsi Azam, haikushangazwa juu ya suala hilo kupata nafasi nne kwa kuwa tayari tulishajiandaa mapema kushiriki michuano ya kimataifa kupitia ubingwa wa ligi kuu au Kombe la Shirikisho, hivyo hata kama hizo nafasi zisingekuwepo bado sisi malengo yangekuwa hivyo ndiyo maana tunaendelea kupambania ubingwa,” .

 Yanga wanasemaje?

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Young Africans, Hassan Bumbuli, amebainisha kwamba: “Kitu ambacho huenda hakifahamiki ni kwamba Young Africans ipo kwenye malengo makubwa ya kucheza michuano ya kimataifa, lakini siyo kwa sababu ya hizo nafasi za upendeleo.

“Kitu pekee ambacho tunachokiamini ni kushinda ubingwa wa ligi kuu au Kombe la FA ili tuweze kupata nafasi ya uhakika, lakini siyo hiyo ambayo imekuwa ikitajwa.”

Msiruhusu wahamiaji haramu kuingia kiholela - Jenerali Mbuge
Watatu hatarini kuikosa Dodoma Jiji FC