Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’ limethibitisha kupokea vibali vya wachezaji wa Kigeni wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans, ikiwa ni saa chache baada ya kutoa taarifa ya kupokea vibali vya Azam FC pekee.

TFF imethibitisha kupokea vibali hivyo kwa taarifa rasmi iliyochapishwa katika vyanzo vyake vya habari, huku ikiweka wazi majina ya wachezaji 12 wa kigeni wa Young Africans waliopata vibali.

Wachezaji hao ni  Djigui Diarra, Jesus Moloko, Stephane Ki Aziz, Joyce Lomalisa, Khalid Aucho, Kennedy Musonda, Koussi Yao, Gift Fred, Mahlatse Makudubela, Hafiz Konkon, Max Mpia na Zouzoua Peodoh.

Simba SC wafunguka ishu ya Moses Phiri
Young Africans: Tumeona taarifa ya TFF, watacheza