Kiungo wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Thadeo Lwanga, hatokuwa sehemu ya kikosi cha Timu ya Taifa ya Uganda (The Cranes), inayokabiliwa na michezo ya kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Kenya na Mali.

Kocha Mkuu wa The Cranes Milutin Srendojevic ‘Micho’ amethibitisha taarifa za kiungo huyo, ambaye amepata majeraha yatakayomuweka nje kwa kipindi chote ambacho Uganda itakua kwenye harakati za kusaka alama tatu dhidi ya Kenya na Mali.

Kocha Micho amesema amefadhaishwa sana na taarifa za kuumia kwa kiungo huyo wa klabu ya Simba, na amemtakia kila la kheri katika kipindi ambacho atakua anajiuguza kabla ya kurudi dimbani.

“Nimefadhaika sana kusikia taarifa za kuumia kwa Thadeo Lwanga, nilitarajia kumtumia kikamilifu katika michezo itakayotukabili hivi karibuni, sina budi kumuombea ili apone kwa haraka na kurudi tena uwanjani.” amesema Micho.

Lwanga alikuwa sehemu ya kikosi cha Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba SC, kilichokuwa kambini nchini Morocco, kabla ya kurejea Dar es salaam Jumamosi (Agosti 28).

Azam FC yapata mteremko kimataifa
GMS: Msiihukumu Young Africans kwa mchezo mmoja