Hitaji na klabu ya Tottenham la kumsajili kiungo kutoka nchini Ufaransa na klabu ya Valencia ya Hispania Geoffrey Kondogbia, limeongezewa changamoto, baada ya viongozi wa Els Taronges (The Oranges) kusisitiza mchezaji huyo hatouzwa chini ya Euro milioni 70.

Spurs bado hawajafanya usajili wa mchezjai yoyote katika kipindi hiki cha dirisha la usajili wa majira ya kiangazi, na tegemo lao la kwanza limewekwa kwa kiungo huyo.

Tayari mwenyekiti wa klabu hiyo ya jijini London Daniel Levy ameshajaribu kuomba mazungumzo na uongozi wa Valancia CF, lakini sharti la kwanza alilopewa ni msisitizo wa bei itakayotumika katika bishara ya usajili wa Kondogbia.

Kondogbia, mwenye umri wa miaka 25, alijiunga na klabu hiyo ya Hispania mwaka 2017 kwa mkopo na mwanzoni mwa mwaka huu 2018 alisajiliwa jumla akitokea Inter Milan ya Italia.

Endapo kiungo huyo atasajiliwa, changamoto ya ushindani itaongezeka katika eneo la kati kati la kikosi cha Spurs ambalo kwa sasa linawashugulisha wachezaji Eric Dier na Victor Wanyama.

Pamoja na msisitizo wa bei ya Euro milioni 70 kuwekwa wazi na uongozi wa Valencia CF, mpaka sasa hakuna taarifa zozote kutoka Spurs ambazo zinadhihirisha kama wapo tayari kuendelea na mazungumzo ya usajili wa kiungo huyo.

Mkuu wa Wilaya ya Hai aapishwa
Mahakama yamnyooshea kidole Mbowe