Mlinda Mlango na Nahodha wa timu ya taifa ya Uganda (The Cranes) Denis Onyango amemtaka Rais wa nchi hiyo Yoweri Kaguta Museveni kutekeleza ahadi yake ya kuipatia timu ya taifa Dola Milioni 1 (sawa na Bilioni 2 za kitanzania).

Mchezaji huyo mwenye umri miaka 35 alikuwa sehemu ya kikosi ambacho kiliweka historia kwa Taifa la Uganda kufika hatua ya mtoano katika fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2019).

Rais Museveni alitoa ahadi hiyo Ikulu ya Entebbe mnamo Julai 8, 2019, baada ya Cranes, chini ya kocha Mfaransa Sebastien Desabre kufanya vyema na kufika hatua ya mtoano. Uganda iliondolewa na Senegal katika Raundi ya 16, wakilala kwa bao 1-0.

Kipa huyo anaeitumikia klabu ya Mamelodi Sundowns inayoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini, amemkumbusha Rais Museveni kutimiza ahadi yake, wakati wa akimtakia kheri ya siku yake ya kuzaliwa kwa kutimiza miaka 76.

“Unavyozeeka vizuri, sisi kama vijana wa Uganda Cranes tunakosa jinsi ya kuku-surprise,” – Onyango kwenye ukurasa wake rasmi wa Facebook.

“Lakini Bado unaweza kurudisha neema na ukafanya vizuri kwa kutimiza ahadi yako ya mwaka jana ya kutuzawadia $ milioni 1 kwa juhudi zetu nzuri kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2019).

“Vijana wako wanahitaji sana katika nyakati hizi ngumu za majanga! Kwa mara nyingine tena, Happy Birthday Mr President.”

Nyota wengine wa Uganda The Cranes waliomtakia kheri ya siku ya kuzaliwa Rais Museveni ni Farouk Miya na Tadeo Lwanga, na kumtaka atimize ahadi yake

“Kama nahodha, wachezaji wenzangu (wengine tayari wamestaafu sasa) wamefika kwa unyenyekevu wakiniuliza [wengine kwa sauti ya kudai kwa sababu wameanza kukata tamaa] mimi naomba nikukumbushe ahadi hiyo.”

Spurs kumrejesha Gareth Bale?
Patrice Carteron akabidhiwa mikoba Al-Taawon