Mahakama ya Kimataifa ya Haki The Hague hii leo inatarajiwa kutoa uamuzi wa kesi ya muda mrefu kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Uganda ambapo nchi zote mbili zinadai zilipwe fidia kutokana na mizozo katika jimbo la Ituri lenye utajiri wa madini nchini DR Congo kuanzia mwaka 1998 hadi 2003.

Mwaka 2005, mahakama iliamua kwamba Uganda lazima ilipe fidia kwa DR Congo kwa kukalia na kupora mali huko Ituri ambapo iligundua kuwa DR Congo ina hatia ya kushambulia ubalozi wa Uganda katika mji mkuu Kinshasa na kuuamuru ulipe fidia.

Mahakama iliamuru majirani hao kujadiliana kuhusu fidia lakini hawakuweza kufikia makubaliano, huku Kinshasa ikirejesha kesi hiyo mahakamani mwaka wa 2015.

DR Congo inadai zaidi ya $11bn (£8bn) kama fidia kwa kuikalia Uganda, ambayo imekataa na kutaja hatua hiyo kama”isiyo na uwiano.”

Katika matukio hayo ya nchi za mashariki mwa Afrika, huko Burundi EU imeiondolea nchi hiyo vikwazo vya kifedha

Taarifa zinasema Rais Évariste Ndayishimiye afurahishwa na uamuzi wa EU wa kuondoa vikwazo.

EU imetaja mazingira ya amani ya kisiasa na maendeleo ya serikali ya Burundi katika maeneo kadhaa, ikiwa ni pamoja na haki za binadamu na kurejea kwa hiari kwa wakimbizi nchini humo.

Hata hivyo ilibainisha kuwa changamoto zinazoendelea zimesalia “katika nyanja za haki za binadamu, utawala bora, maridhiano na utawala wa sheria.“

Kuondolewa kwa vikwazo na EU kunafuatia uamuzi kama huo wa Marekani mwaka jana. Vikwazo hivyo viliwekwa mwaka wa 2016 baada ya hayati Rais Pierre Nkurunziza kugombea muhula wa tatu madarakani, jambo ambalo lilizusha maandamano mabaya ya watu mitaani.

Wachezaji Simba SC kuikosa ASEC Mimosas
Milionea aliyeendesha gari kwa kasi zaidi ashtakiwa kwa makosa ya barabarani