Klabu ya Newcastle United imerejea ligi kuu ya England baada ya kuwashushia kisago cha mbwa mwizi Preston North End cha mabao 4-1 huko St James’ Park katika mchezo uliochezwa usiku wa kuamkia leo.

Mabao yaliyoirejesha Newcastle United ligi kuu England yalifungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Hispania, Ayoze Perez aliyefunga mabao mawili katika kipindi cha kwanza na cha pili.

Mabao mengine yalifungwa na Christian Atsu pamoja na Matt Ritchie aliyefunga kwa mkwaju wa penati baada ya nahodha wa Preston North End, Paul Gallagher kuushika mpira kwa makusudi ndani ya eneo la hatari. Bao la kufutia machozi la Preston North End lilikwamishwa wavuni na Jordan Hugill.

Ushindi huo umeirejesha Newcastle United ligi kuu ya England, ikiwa ni baada ya ni siku 348 zimepita tangu iliposhuka daraja msimu uliopita pamoja na vilabu vya Norwich City pamoja na Aston Villa.

Waamuzi Ligi Kuu Tanzania Bara Wapewa Onyo
Live: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Aprili 24, 2017