Taasisi ya The think tankers of Tanzania imesema kuwa imefadhaishwa sana na taarifa iliyotolewa na ubalozi wa Marekani hapa nchini, ambapo imesema kuwa ingawa Tanzania ni nchi ndogo lakini inapaswa kuheshimiwa na inawashukuru kwa kuonyesha kuwajali.

Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Peter Msaki alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema kuwa Ubalozi huo ulitakiwa kujirisha kwanza kabla ya kutoa taarifa lakini kwa ukubwa wa Taifa la Marekani na uzoefu wao katika serikali kusambaza barua mitandaoni kabla ya kuipeleka Wizara ya Mambo ya Ndani na Tume kumeshangaza na kunashusha hadhi ya wafanyakazi wa ubalozi huo.

“Taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Marekani ni kama imeandikwa na Chama kimoja cha Upinzani halafu Ubalozi wa Marekani ukatumika kuisambaza!

Haipo kidiplomasia ipo kisiasa zaidi.” Amesema Msaki

Aidha, ameongeza kuwa tabia ya Marekani kutoa taarifa pasipo na kujiridhisha zimeliletea maafa makubwa bara la Afrika huku akitolea mfano wa Libya

Hata hivyo, Msaki ameongeza kuwa, Jeshi la polisi halimkamati mtu kwasababu ya itikadi zake za kisiasa bali linamkamata mtu kwa makosa yake.

“Jeshi la polisi halimkamati mtu kwasababu ya Itikadi yake ya Kisiasa bali linamkamata mtu kwa makosa yake ya kuvunja Sheria na ndio maana wanapomkamata mtu hawaulizi Chama wala kadi ya Chama na pia haliwezi kukuacha uvunje sheria kwasababu wewe ni Mwanasiasa” Amesema Msaki

Pia, Mwenyekiti huyo wa The think tankers of Tanzania amesema kuwa; “Tunawapenda sana Wamarekani, ni ndugu na marafiki zetu na wamekuwa wabia wakubwa wa maendeleo katika Taifa letu, tunaamini Ubalozi wao kwa bahati mbaya uliteleza kidogo.”

Video: Waziri Lugola aagiza vigogo NIDA wakamatwe
Wagonjwa 19 wanufaika na matibabu ya Figo