Mlinda mlango wa klabu ya Southampton Fraser Forster, amelazimika kuondoka kwenye kambi ya timu ya taifa ya England, kufuatia majeraha ya mkono yanayomkabili.

Kikosi cha England kiliingia kambini mwanzoni mwa juma hili, tayari kwa maandalizi ya mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia za mwaka 2018 dhidi ya timu ya taifa ya Slovakia ambao utachezwa siku ya jumapili.

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya England Sam Allardyce, amethibitisha kuondoka kwa mlinda mlango huyo, na amaeahidi kujaza nafasi yake kabla ya kikosi chake hakijaelekea katika mtanange huo ambao utachezwa nchini Slovakia.

Forster, tayari amesharejea Southampton kwa ajili ya kuanza matibabu ambayo hayajaelezwa yatachukua muda gani mpaka atakaporejea tena katika hali yake na kukaa langoni.

Kuondoka kwa mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 28, kunamaanisha kikosi cha England kinasaliwa na Joe Hart ambaye tayari amesharejea jijini London akitokea mjini Turin nchini Italia, alipokua amekwenda kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kujiunga na klabu ya Torino kwa mkopo akitokea Man City.

Kama Mambo Yangekwenda Vizuri, Sturridge Angetua Emirates Stadium
‘Bunge’ lamtimua madarakani Rais wa Brazil