Wakati Liverpool ikiwa tayari kumuachia kiungo wake kutoka nchini Hispania Thiago Alcantara, baada ya kupata ofa kutoka Saudi Arabia, imefahamika kuwa mchezaji huyo amegoma kuondoka.
Thiago amekataa mpango wa yeye kuondoka ndani ya Liverpool kwenda kujiunga na moja ya timu kutoka Saudi Arabia licha ya kuwekewa mkwanja mrefu.
Saudi Arabia imeendelea na mpango wake wa kusajili mastaa kutoka Ulaya katika klabu tofauti ambapo baadhi ya wachezaji waliotua huko kuelekea msimu ujao ni Roberto Firmino, Karim Benzema na N’Golo Kante.
Liverpool wapo tayari kumuuza kiungo huyo aliyebakiwa na mkataba wa mwaka mmoja ili kufanikiwa kumsajili Romeo Lavia kwa Pauni 50m ambaye atakuwa mbadala wake.
Kwa sasa Liverpool ipo katika mazungumzo ya kumsajili Lavia kutoka Southampton.
Ikumbukwe kuwa, Liverpool ilimsajili Thiago Alcantara Septemba 18, 2020 kutoka FC Bayern Munich.
Kiungo huyo katika muda wake wa misimu mitatu, amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara.