Mlinda Lango kutoka nchini Ubelgiji na klabu ya Real Madrid ya Hispania Thibaut Courtois ameonesha kufurahia na taarifa za kurudi jijini London kwenye Uwanja wa Stamford Bridge wakati klabu yake itakapomenyana na Bingwa Mtetezi Chelsea katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya.

Wababe hao walikutana hatua ya nane bora katika marudio ya nusu-fainali ya msimu uliopita 2020/21, ambapo Chelsea ilishinda mabao 3-1 na kutinga hatua ya Fainali dhidi ya Man City.

Courtois alicheza katika michezo yote miwili, pamoja na sare ya nyumbani iliyochezwa kwenye Uwanja wa Alfredo Di Stefano.

Mashabiki wa The Blues hawakufurahishwa na jinsi Courtois alivyoondoka, lakini kipa huyo anaangazia zaidi mataji mawili ya Ligi Kuu na makombe mawili ya nyumbani aliyoshinda akiwa na klabu hiyo.

Iwapo watapitia, Chelsea itakuwa timu ya kwanza ya England kuwaondoa Real Madrid kwenye Ligi ya Mabingwa mara kadhaa.

Los Blancos wamekutana na Chelsea mara nyingi bila kushinda kuliko walivyocheza na timu nyingine yoyote kwenye mashindano ya Ulaya, sare mara mbili na kupoteza mara tatu.

Kocha Pablo: Wachezaji wapo tayari kuivaa USGN
Young Africans kuivaa Azam FC kwa mbinu mpya