Mlinda mlango wa klabu ya Chelsea Thibaut Courtois amesema kama Chelsea wanataka kutetea ubingwa wa EPL basi ni lazima wapate ushindi dhidi ya Manchester United katika mchezo wa ligi kuu utakaopigwa Jumapili.

Chelsea ambao wako katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa EPL wakiwa na pointi 19 baada ya kucheza michezo 10 watawakaribisha Manchester United katika uwanja wa Stamford Bridge Jumapili.

”Manchester City wana pointi 9 zaidi yetu, Man Utd wanatuzidi pointi 4 na Tottenham pointi moja, tunatakiwa kushinda michezo ya aina hii ili kupunguza tofauti ya pointi na wapinzani wetu,” alisema Thibaut Courtois.

Ni mchezo mmoja tu ambao Chelsea wamecheza bila kuruhusu kufungwa goli na hapo jana katika mchezo dhidi ya As Roma kwenye michuano ya klabu bingwa barani Ulaya Chelsea walipokea kichapo cha mabao 3-0.

Mshambulia wa Roma El Shaarawy scored alimfunga mabao mawili Courtois kabla ya Diego Perotti kufunga bao la tatu dakika ya 63 na kupeleka kilio kwa kikosi hicho cha Antonio Conte.

 

Video: Makonda awaalika wapinzani…
Haji Manara amjibu mchambuzi wa soka Tanzania