Nyota wa zamani wa Ujerumani, Dietmar Hamann amedai kuwa Meneja wa saw a FC Bayern Munich, Thomas Tuchel huenda akafutwa kazi kama klabu hiyo itashindwa kutwaa taji la Bundesliga msimu huu 2022/23.
Tuchel mwenye umri wa miaka 49, aliteuliwa kuwa Meneja wa FC Bayern Munich kufuatia kuondolewa kwa Julian Nagelsmann mwezi Machi na amekuwa na matatizo katika kipindi kifupi alichokuwa Allianz Arena hadi sasa.
Tuchel alishinda mchezo wake wa kwanza dhidi ya klabu yake ya zamani Borussia Dortmund, lakini Bayem tangu wakati huo imepoteza nafasi ya kwanza kwa Dortmund, pamoja na kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya na Kombe la Ujerumani DFB Pokal.
Bayern walichapwa 3-1 na Mainz siku ya Jumamosi (April 22), huku Dortmund wakiwaruka katika kilele cha Bundesliga kufuatia ushindi wa 4-0 dhidi ya Frankfurt.
Ripoti kutoka Ujerumani zimedai Bodi ya Bayern chicni ya Mkurugenzi Mtendaji Mkuu, Oliver Kahn na Mkurugenzi wa Michezo, Hasan Salihamidzic itakutana Mei 22 ili kuamua mustakabali wa Tuchel.