Kituo cha Uwekezaji Tanzania – TIC, kimesema kimetoa huduma kwa miradi 1,038 ya wawekezaji sawa na asilimia 81.7 kati ya miradi 1,270 iliyoisajili katika kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2018 hadi 2022.

Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Gilead Teri ameyasema hayo katika ripoti ya uwekezaji ya kila mwezi ya kituo hicho kwa Machi mwaka huu.

Amesema, mafanikio hayo yalichangiwa na ushirikiano uliopo kati ya wadau, wawekezaji na kituo katika kushughulikia changamoto mbalimbali za upatikanaji wa vibali, uidhinishaji, ardhi, leseni na masuala ya kodi.

“Serikali itaendelea kuhakikisha mazingira ya biashara na uwekezaji yanaboreshwa ili kuvutia zaidi uwekezaji wa ndani na wa nje,” alisema Teri.

Aidha, ameongeza kuwa, katika kipindi cha Machi 2023 TIC ilitoa huduma kwa miradi 1,247 ya wawekezaji ikiwamo kuitembelea ikilinganishwa na huduma iliyotolewa kwa miradi 122 Februari 2023.

Vinicius Junior: Ancelotti anafaa kuinoa Brazil
Hitimana: Nilijua kuna siku ningeondoka KMC FC