Aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Habari Tanzania (TBC), Tido Mhando amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka matano.
Tido ambaye alifika mahakamani hapo leo majira ya saa tano anakabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi, matumizi mabaya ya ofisi yake na kuisababishia hasara Serikali ya shilingi milioni 887.
Mwanahabari huyo nguli alisomewa mashtaka yake matano katika mahakama ya wazi na kuendelea na taratibu nyingine za kimahakama.
Tido alishika madaraka ya ukurugenzi wa TBC akitokea jijini London Uingereza alipohudumu kama mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC, alipohudumu tangu mwaka 1999.
- Video: Hata wanaomtukana Rais watatibiwa hapa- RC Makonda
- Mbowe, Lowassa kumnadi Salum Mwalimu kesho
Hivi sasa, Tido anaiongoza Azam Media na amefanikiwa kukipa umaarufu kipindi chake cha ‘Funguka’ ambapo amekuwa akiwahoji viongozi mbalimbali hasa wa kisiasa.