Mtoto wa Diamond Platinumz, Tiffah ameundiwa kamati maalum kwa ajili ya kuratibu shughuli ya sherehe yake ya kufikisha siku arobaini tangu azaliwe, inayotarajiwa kufanyika Jumapili, Septemba 20.

Kwa mujibu wa gazeti la Nipashe, mama mzazi wa Diamond ndiye anayeongoza kamati hiyo yenye wajumbe kadhaa ambao ni ndugu wa karibu wa familia ya mwimbaji huyo.

“Tiffah anatutoa jasho shangazi zake, mimi na wanakamati wenzangu tunaendelea kujumuika pamoja, kwa ajili ya Tiffah inabidi na sisi tufutwe jasho Jumapoli kwa kweli,” Esma ambaye ni mdogo wake Diamond ananukuliwa.

Pamoja na Esma na Mama Diamond, wengine wanaouna kamati hiyo ni mama mzaa chema, Zarina ‘The Bosslady’ Hassan.

Sura ya Tiffah inatarajiwa kuoneshwa kwa mara ya kwanza hadharani siku hiyo ya Jumapili, Septemba 20.

Dimond aliandika ujumbe wa kuwafahamisha mashabiki wake kuhusu siku hiyo.

On the 20th of September 2015 my Daughter’s face @princess_tiffah will be Exclusively shown for the first time to the public… would you like to know which companies have sponsored her first video and photo??? Apart from being @MsasanicityMall and @PuguMall #BABYSHOP brand Ambassador would you like to know which companies have endorsed her??? Stay with me!!! #TIffahsDay Coming Soon..% (Tareh 20|09|2015 kwa mara ya kwanza sura ya Binti yangu @princess_tiffah tutaiweka hadharani…je ungependa kujua ni Kampuni gani imedhamini Video na Picha yake ya kwanza????.. Mbali na kuwa balozi wa #BABYSHOP ya @Msasanicitymall & @Pugumall ungependa kujua amekuwa Balozi wa nini tena???.. uskae mbali na mimi… #TiffahsDay inakaribia..%) #ProudDad

A photo posted by Chibu Dangote..? (@diamondplatnumz) on

Mourinho: Inatosha Kufungwa Nyumbani
Alichofanya Tibaijuka Baada Ya Mpiga Debe Wake Kuteleza ulimi...