Chama cha Wamiliki wa Mabasi (TABOA), kimejipanga kuanza kukata Tiketi kwa njia ya  ya Kielektroniki kuanzia mwezi Februari mwaka huu kwa kampuni zote za mabasi ili kukabiliana na msongamano unaojitokeza.

Katibu wa chama hicho, Enea Mruto amesema, baada ya kufanya kikao na Mamlaka ya Mapato (TRA), wamefikia muafaka wa kuanza kutumia Mfumo wa Kielektroniki kwa mabasi yote

“Kama TRA hawatatuangusha kwa  kile tulichokubaliana nao, basi mpango huo utaanza rasmi mwezi ujao, tunahitaji kufanya kazi kwa kwenda na kasi ya teknolojia mpya”alisema Mruto.

Amesema utaratibu huo ulianza katika baadhi ya kampuni za mabasi, utatumika katika kampuni zote za mabasi baada ya kukamilika kwa baadhi ya mambo waliyokubaliana kisha utazinduliwa rasmi na kuwekwa agizo kwa mabasi yote.

Ameongeza kuwa kupitia mfumo huo, wateja watapata tiketi kirahisi na vilevile wataweza kuweka maombi kwa njia ya mtandao.

TABOA imesema inatekeleza agizo la Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na mawasiliano Atashata Nditiye kuhusu kuzingatia leseni zao katika usafirishaji wa vipeto(sandarusi) kwenye mabasi.

Pamoja na hayo, Mruto ametoa wito kwa kampuni za mabasi hususani madereva kuwa makini ili kuepusha Ajali za Barabarani. Pia, ameshauri wamiliki kuhakikisha mabasi yanafanyiwa ukaguzi mara kwa mara.

Wanafunzi waliofanyia mtihani gerezani wafaulu kwa kishindo
Mvua zatajwa kutosaidia joto kushuka nchini